WAMA YAKANUSHA TAARIFA ZILIZOANDIKWA KATIKA MAGAZETI KUHUSU MAMA SALMA KIKWETE, SOMA HAPA

WAMA yakanusha taarifa iliyoandikwa kwenye gazeti kuhusu Mama Salma Kikwete

img_20161202_212521

KAULI YA TUME YA WATUMISHI WA UMMA KUHUSU UDHALILISHAJI WA WATUMISHI WA UMMA, SOMA HAPA

Tume ya Utumishi wa Umma imetaja mamlaka sita zenye dhamana na madaraka ya kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi wa umma kisheria ikiwa pamoja na kufuta nafasi za madaraka.

Vilevile, Tume hiyo imezitaka mamlaka za nidhamu zote kuzingatia sheria, kanuni pamoja na taratibu wakati wa kutekeleza majukumu yao kwani kwa kufanya hivyo, watumishi wanaotuhumiwa kufanya kosa watatendewa haki.

Tume ya Utumishi wa Umma imetoa maelekezo hayo siku chache baada ya viongozi wengi katika Serikali ya Awamu ya Tano wakiwamo wakuu wa mikoa na wilaya kuwachukulia kiholela hatua za nidhamu watumishi wa umma wakati baadhi hawana mamlaka hayo kisheria.

Baadhi ya wakuu wa mikoa wamekuwa waki- wasimamisha watumishi hadharani tena kwa kusikiliza malalamiko ya upande mmoja bila kuwapa walalamikiwa nafasi ya kujitetea, na wakati mwingine kudhalilishwa katika mikutano.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu Msaidizi Tume hiyo, Enos Mtuso alisema kwa kuzingatia Sheria ya Utumishi wa Umma Na 8 ya mwaka 2002 na kanuni zake za mwaka 2003 madaraka ya kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi wa umma yako chini ya watu wachache.

“Sheria ya Utumishi wa Umma Na 8 ya mwaka 2002 ilitungwa ili kuweka misingi ya kisheria katika kutekeleza malengo ya Sera ya Menejimenti na Ajira katika Utumishi wa Umma iliyopitishwa na Serikali mwaka 1998.

Sheria hii ndiyo inayotoa uwezo kwa mamlaka za kinidhamu mbalimbali katika utumishi wa umma na kuweka misingi ya namna masuala hayo yanavyopaswa kushughuliwa,” alisema.

Mtuso alizitaja mamlaka hizo kuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), Katibu Mkuu Kiongozi, watendaji wakuu, wakuu wa idara na divisheni, na mamlaka za Serikali za Mitaa (Baraza la Madiwani).

Lakini alipoulizwa mkuu wa mkoa anapata wapi mamlaka ya kuwafukuza kazi watumishi wa umma na kuwadhalilisha mbele ya hadhara, Mtuso alisema wao kama Tume hawana mamlaka ya kuzungumzia jambo hilo kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wanakiuka maadili na kwamba suala hilo liko chini ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Kauli ya Tume iliwekewa uzito na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), Seleman Jaffo ambaye amewataka wakuu wa idara kuacha kuwanyanyasa wafanyakazi kwani hali hiyo inasababisha wafanye kazi kwa hofu ya kutumbuliwa.

Akizungumza baada ya kuwatembelea watumishi wa umma wa Manispaa ya Ilala, jijini Dar es Salaam jana, Jaffo alisema wizara yake itatoa ushirikiano kwa watumishi wote wanaofanya kazi kwa bidii.

Katika hatua nyingine, Mtuso alitoa takwimu za mashauri ya nidhamu yaliyochukuliwa hatua katika kipindi cha 2014/2015 na 2015/2016 akisema jumla ya watumishi wa umma 249 sawa na asilimia 75 ya mashauri yote yaliyowafikia wakiwamo walimu 209 walifukuzwa kazi kwa makosa yaliyothibitika.

 Alisema Watumishi hao wamefukuzwa kazi kwa makosa mbalimbali ikiwamo, kukiuka maadili ya kazi, kutotekeleza majukumu, ubadhilifu, rushwa, wizi wa fedha na mali, udanganyifu, matumizi mabaya ya madaraka, uzembe, utovu wa nidhamu huku utoro kazini ukiwa na idadi kubwa ya waliofukuzwa kazi.

“Utoro kazini ni changamoto kubwa inayotukabili na ndiyo mashauri yake mengi yanathibitika, unakuta mtumishi haendi kazini siku tano na kuendelea bila sababu maalumu wala hatoi taarifa yoyote kwa waajiri wake kuwa anashida gani,” alieleza.


LEMA AIAGA RASMI FAMILIA YAKE, ASEMA YUPO TAYARI KUKAA GEREZANI HADI DOLA ITAKAPOAMUA.. SOMA HAPA

Baada ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kukwama tena kupata dhamana mahakamani jana, amewataka mawakili wake kutomhangaikia na kuliacha suala hilo kama lilivyo na atakaa gerezani hadi Januari mwakani.

 Akizungumza baada ya Mahakama Kuu kuondoa rufaa ya mbunge huyo aliyekuwa akipinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kumnyima dhamana, Wakili wa Lema, John Malya alisema mteja wake amewaomba kutokata tena rufaa na kuiachia Jamhuri iamue inavyotaka.

“Baada ya kujadiliana na mbunge, tumeona tufuate kwanza maelekezo yake ya kutofanya lolote juu ya maombi mapya ya dhamana,” alisema Malya.

Kutokana na maombi ya dhamana yake kukwama, Lema alirejeshwa kwenye Gereza la Kisongo ambako ataendelea kuwa mahabusi kusubiri hatima ya kesi inayomkabili.

“Tulikuwa na njia nyingi za kufanya kwa ajili ya kudai haki ya dhamana ya Lema lakini mbunge ameshatoa agizo hilo,” alisema Malya.

Aidha mke wa Lema, Neema Lema alisema amejadiliana na mumewe na kuona kinachoendelea kwenye shauri la kesi hiyo.

“Wanasheria walitoa ushauri wa nini kifanyike lakini mume wangu ameamua kisifanyike chochote kuanzia sasa. Pamoja na yote yanayotokea sasa ifike mahala ieleweke kuwa nchi si mali ya mtu yeyote, bali ni mali ya Watanzania wote,” alisema Neema.

Lema  alikamatwa Novemba 2, akiwa bungeni Dodoma na kurejeshwa Arusha kujibu mashtaka ya kutoa kauli za uchochezi namba 440 na 441/2016.

Katika kesi hiyo, anadaiwa kuwa kati ya Oktoba 23 na 26 alitoa kauli za uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli katika maeneo tofauti wakati wa mikutano yake ya hadhara.

Tangu wakati huo mawakili wake wamejitahidi bila mafanikio kumtoa kwa dhamana na ndipo baadaye walikata rufaa Mahakama Kuu ambako pia imeshindikana kwa maelezo kuwa iliwasilishwa nje ya muda wa siku 10 unaotakiwa kisheria.

Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Angelo Rumisha akisoma uamuzi wa Jaji Mfawidhi, Fatuma Masengi alitaja sababu za kuondolewa rufaa hiyo kuwa ni mshtakiwa kushindwa kuonyesha kusudio la kukataa rufaa ndani ya muda. Pia, alisema Mahakama Kuu inafungwa mkono kutoa uamuzi mwingine.

Rumisha alisema mshtakiwa alipaswa kuwasilisha notisi ya kukata rufaa hiyo ndani ya siku 10, tangu uamuzi wa Mahakama ulipofanyika lakini badala yake upande wa utetezi ulikata rufaa nje ya siku 10.

“Maamuzi yalifanyika tarehe 11 , ilipaswa hadi Novemba 21 wawe wameonyesha kusudio la kukata rufaa lakini walikata rufaa tarehe 22,” alisema Msajili.

“Mahakama inaungana na pingamizi la Jamhuri, hivyo imeiondoa rufaa hii,” alisema.

Awali, Jamhuri ndiyo iliweka pingamizi, kupitia mawakili wake, Paul Kadushi na Matenus Marandu ikipinga kusikilizwa kwa maombi ya rufaa hiyo ya Lema iliyowasilishwa na wakili Peter Kibatala kwa maelezo imekiuka sheria.

Wakili Marandu alisema Kifungu cha Sheria 361 (1)(a) cha Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) kinataka mkataji rufaa kuonyesha nia ya kukata rufaa kwa kuandika notisi ya rufaa hivyo kuitaka Mahakama itupilie mbali rufaa hiyo.

Chadema wasikitika
Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini na Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Amani Golugwa alisema kutokana na uamuzi huo, kwa sasa wanaheshimu uamuzi wa Lema kuiachia Jamhuri kuamua hatima yake.

“Tumefedheheshwa sana na kitendo Msajili alichokifanya kuwa kama Lema ataongea mawakili wake watoke nje na kama haiwezekani asubiri mpaka pale atakapomaliza kusoma maamuzi,” alisema Amani

Wakati Msajili akitaka kusoma uamuzi huo jana saa 3:50 asubuhi, Lema alinyoosha mkono akiashiria kutaka kuongea lakini hakupewa ruhusa na Msajili. Badala yake alisema mawakili wake ndiyo walipaswa kutoa hoja ya mshtakiwa huyo kwamba kama Lema ataongea itabidi mawakili wake watoke nje.

Baada ya uamuzi kufanyika, Wakili wa Lema Adam Jabir alisimama na kutoa hoja ya mbunge huyo kumuomba Msajili awaruhusu ndugu zake mshtakiwa waingie ndani ya Mahakama kusikiliza shauri lake baada ya kuzuiwa na Jeshi la Polisi.

Msajili alijibu kuwa mahakama haina fedha za kununua vipaza sauti. Pia, alisema wamezuia watu wengine kuingia kwenye Mahakama hiyo kwa kuwa eneo hilo ni dogo. Lema amerudishwa mahabusu huku kukiwa na sintofahamu ya lini rufaa ya kupinga dhamana yake itasikilizwa.

VIDEO, MCHEKESHAJI ERIC OMONDI ALIVYORUDIA WIMBO WA SOUT SAUL 'KULIKO JANA' TAZAMA HAPA

Miongoni mwa wakali wa Comedy huwezi kuacha kumtaja Eric Omondi kutokea Kenya ambaye huwa anafanya covers mbalimbali za nyimbo za wasanii hasa zinazotrend, ameirudia kivingine ‘Kuliko jana’ ya Sauti Sol ambapo ameipa title ya ‘kuliko jana Refix’.

Unaweza kutazama kwa kubonyeza play hapa chini, ukishaitazama usiache kuniachia comment yako.

VIDEO.. WATOTO WA LEMA WAKIMUAGA BABA YAO KWA UCHUNGU BAADA YA KUKOSA DHAMANA, TAZAMA HAPA


Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema amekosa tena dhamana leo December 2 2016 na kurudishwa rumande kwenye kesi inayomkabili ya kutoa maneno ya uchochezi kwa viongozi wa nchi akiwemo Rais.
Miongoni mwa waliokuwepo Mahakamani ni familia yake Mke na Watoto ambao walimpungia wakati akiondoka Mahakamani hapo, unaweza kutazama hii video fupi hapa chini…

TAARIFA MPYA KUTOKA IKULU KUHUSU BOSS WA MAGEREZA, SOMA HAPA

AJALI 8 ZA NDEGE ZILIZOTIKISA ULIMWENGU WA SOKA. SOMA HAPA

Katika wiki hii Ndege iliyokuwa imebeba timu ya soka ya Brazil ilianguka wakati ilipokuwa ikikaribia mji wa Medellin nchini Colombia na karibu watu wote 81 waliokuwa ndani yake kuuwa kwa ajali hiyo ambayo baadae ilijulikana ni kwasababu iliishiwa mafuta.

Ndege hiyo ilikuwa na wachezaji wa timu ya Chapecoense, waliokuwa safarini kwenda kucheza fainali ya Mashindano ya Kimataifa ya Vilabu vya Amerika ya Kusini.

Chapecoense ndiyo klabu ya hivi karibuni kukumbwa na mkasa kama huo.

Mikasa mingine kama hiyo iliyowahi kutokea ni:

 Il Grande Torino – 1949

Mwezi Mei mwaka 1949 ndege iliyokuwa imeibeba timu ya Torino ilianguka eneo la milima iliyoko karibu na Turin na kuwaua watu 31.

Wakati huo timu ya “Il Grande Torino” ilikuwa klabu kubwa nchini Italia baada ya kupata ushindi mara tano.

Kablu hiyo hikuweza kujikwamua kufuatia ajali hiyo ambayo iliangamiza karibu kikosi chote.

Ajali ya Munich – 1958
Ndege iliyokuwa imebeba timu ya Manchester United ilianguka mjini Munich

Ndege iliyokuwa imebeba timu ya Manchester United ilianguka mjini Munich

Ndege iliyokuwa imebeba timu ya Manchester United ilianguka mjini MunichNdege iliyokuwa imebeba timu cha Manchester United ambayo kwa wakati huo ilijulikana kama “the Busby Babes” ilianguka ilipokuwa ikipaa wakati timu ikirudi kutoka kuzeza mechi ya bara la ulaya dhidi ya klabu ya Red Star Belgrade. Wachezaji 8 wa United na watu wengine 15 waliaga dunia.

Timu ya kuteleza kwenye theluji ya Marekani – 1961

Wanachama wote 18 wa timu ya kuteleza kwenye theluji ya Marekani walikuwa miongoni mwa watu 73 waliokufa baada ya ndege yao kuanguka karibu na uwanja wa ndege wa Brussels wakati ilipokuwa ikitua.

Timu hiyo ilikuwa safarini kwenda mji wa Prague, huko Czechoslovakia, kushiri katika mashindano na dunia ambayo wakati huo yalifutwa.

Alive – 1972

Siku ya Ijumaa tarehe 13 Oktoba mwaka 1972, ndege iliyokuwa imebeba timu ya Old Christians  na timu ya raga ya Uruguay, ilitoweka ilipokuwa safarini kutoka mji wa Montevideo kwenda Santiago nchini Chile.


Old Christians walionusirika kufa: Pichani ni wao miaka 30 baadae walipokutana nchini Chile. Old Christians walionusirika kufa: Pichani ni wao miaka 30 baadae walipokutana nchini Chile.

Old Christians walionusirika kufa: Pichani ni wao miaka 30 baadae walipokutana nchini Chile.

Miezi miwili baadaye jeshi la wanahewa wa Chile waliwapata manusura 14 kutoka kwa ajali hiyo. Wengine wawili walikuwa wametembea kwa siku 10 na baadae kukutana na wafugaji katika milima ya Andean.

Mkasa huo ulindikwa kwenye vitabu na baadaye kutengenezwa filamu, ALIVE, iliyoeleza jinsi manusura walikula nyama ya binadamu kuepuka kufa na njaa.

FC Pakhtakor Tashkent – 1979

Mwezi Agosti mwaka 1979 wanachama 17 wa timu ya soka la Pakhtakor Tashkent waliuawa wakati ndege yao iligongana na ndege ngingine katika anga ya Ukrain.

Watu wote 178 waliokuwa ndani ya ndege zote mbili waliangamia.

Timu zingine kwenye muungano ya Usovieti zilichangia wachezaji wa klabu hiyo kukiwezesha kumaliza msimu.

Alianza Lima – 1987

Timu ya soka ya Alianza Lima, moja ya vilabu vyenye mafanikio makubwa zaidi ilikuwa ikirejea mjini Lima wakati ndege yao ilianguka kwenda baharini dakika chache kabla ya kutua

Timu yote wa Alianza Lima iliyokuwa miongoni mwa watu 43 iliangamia. Ni rubani tu wa ndege hiyo aliyeweza kunusurika.

Timu ya Soka ya Zambia – 1993

Wanachama 18 wa timu ya taifa ya Zambia waliuawa wakati ndege ya Jeshi la Zambia iliyoanguka karibu na Gabon mnamo tarehe 28 mwezi Aprili mwaka 1993, walikuwa wikielekea kucheza mechi ya kufuzu kwa kombe la dunia nchini Senegal.

Ripoti rasmi kuhusu mkasa huo miaka kumi baadaye ilitaja matatizo ya kimitambo kwenye injini moja ya ndege hiyo.

Timu ya magongo ya Lokomotiv Yaroslavl – 2011

Timu hiyo ambayo ilikuwa ndio mabingwa kwa mfululizo wa mara tatu nchini Urusi ya Lokomotiv Yaroslavl, iliangamia kwenye ajali ya ndege mwezi Septemba mwaka 2011.
Mabaki ya ndege hiyo yaliyopatikana kwenye mto uliokuwa karibu

Mabaki ya ndege hiyo yaliyopatikana kwenye mto uliokuwa karibuMabaki ya ndege hiyo yaliyopatikana kwenye mto uliokuwa karibu

Ndege hiyo ilikuwa ikielekea nchini Belarus kwa mechi ya kwanza ya msimu wakati ilipoanguka na kuwaka moto.

Wachezaji 36 na maafisa waliaga dunia pamoja na wahudumu 7. Mchezaji mwingine aliaga dunia akiwa hospitalini.

MIKOA 10 ITAKAYOKOSA UMEME KESHO JUMAPILI DESEMBA 4, SOMA HAPA

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) linawatangazia wateja wake wa Mikoa ya Dodoma, Singida, Shinyanga, Tabora, Mwanza,  Geita, Mara, Simiyu na na baadhi ya maeneo ya Mikoa ya  Arusha, Manyara, Kilimanjaro  na Tanga na baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Dar es Salaam (Tazara, Mlimani City, Mandela Road, Ubungo na Kimara, Sinza, Mabibo) kuwa yatakosa Umeme siku ya Jumapili Desemba 04, 2016 (Dar es Salaam itakosa umeme Jumamosi pia) kuanzia saa 02:00 Asubuhi hadi saa 11.00 Jioni.

SABABU: Kuruhusu Mkandarasi anayejenga Njia Kuu ya Kusafirisha Umeme ya Msongo Mkubwa ya Kilovolti 400 maarufu kama (Backbone Transmission Line 400 kV) kutoka Iringa hadi Shinyanga.

SABABU: Kuzimwa kwa njia ya Umeme ya Msongo wa Kilovolti 33 Kituo cha Ubungo Dar es Salaam ilikumruhusu Mkandarasi kufanya matengenezo.

Matengenezo hayo yanalenga kuboresha na kuimarisha hali ya upatikanaji wa Umeme Nchini.

Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Imetolewa na;

Ofisi ya Uhusiano

TANESCO Makao Makuu

TAARIFA YA KESI YA GWAJIMA KUHUSU BASTOLA NA RISASI 17, SOMA HAPA

Kesi ya kushindwa kuhifadhi silaha inayomkabili Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima na wenzake watatu imefikia hatua ya kuanza kujitetea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Washtakiwa hao sasa wataanza kujitetea katika mahakama hiyo Desemba 13, 2016 dhidi ya mashtaka yanayowakabili.

Hatua hiyo, imefikiwa baada ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Cyprian Mkeha kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi wa upande wa mashtaka na vielelezo na kuwaona washtakiwa hao wana kesi ya kujibu na wanapaswa kujitetea.

Baada ya uamuzi huo wa Hakimu Mkeha, wakili wao, Peter Kibatala aliiambia mahakama kuwa wateja wake watajitetea kwa njia ya kiapo na wataita mashahidi watatu.

Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo, Hakimu Mkeha alisema siku hiyo watasikiliza ushahidi wa utetezi wa washtakiwa wote wanne na mashahidi wao watatu.

Mbali na Gwajima, washtakiwa wengine ni Askofu Msaidizi, Yekonia Bihagaze, mfanyabiashara Gerge Mzava na mkazi wa Kimara Baruti, Geofrey Milulu.

Awali, shahidi wa kwanza wa upande wa mashtaka, Koplo Sospiter kutoka ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, alidai alikuwa mmoja wa waliomlinda Askofu Gwajima alipokuwa amelazwa Hospitali ya TMJ, Mikocheni chumba namba 213.

Koplo Sospiter aliiomba Mahakama ipokee vitu vilivyokuwamo ndani ya begi linalodaiwa la Gwajima ambavyo ni chupi nyeusi aina ya boksa, suruali mbili, makoti mawili, bastola moja, soksi pea mbili, risasi tatu zilizokuwa katika kasha lake, Ipad moja na CD mbili.

Vingine ni risasi 17 za bastola, vitabu viwili vya kumiliki silaha na hati ya kusafiria ya askofu huyo.

Mahakama ilivipokea kama sehemu ya ushahidi katika kesi hiyo kwa kuwa hakukuwa na pingamizi kutoka upande wa utetezi.

Koplo Sospiter alidai kuwa Machi 28, 2015 mkuu wake wa kazi ambaye ni Mkuu wa Upalelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Constantine Massawe alimpangia kazi ya ulinzi ya kumlinda askofu huyo hospitalini hapo .

Alidai akiwa na askari mwenzake aliyemtaja kwa jina la Ben, Machi 29, 2015, saa tisa usiku, watu watatu ambao ni mshtakiwa wa pili hadi wa nne walifika hospitalini hapo huku mmoja wao akiburuza begi la kijani hadi karibu ya mlango wa kuingilia katika wodi aliyolazwa Gwajima.

Shahidi huyo alidai alipowahoji kilichomo ndani ya begi, walimjibu asitake kujua mambo yao.

Alidai majibu hayo yalimpa shaka na kuhisi kwamba kuna kitu ambacho si cha kawaida, akawasiliana na bosi wake Massawe na kumueleza hali halisi ikiwamo kuomba nguvu ya ziada.

Alidai kuwa ndani ya robo saa lilikuja gari la askari wa doria akiwamo Koplo Magesa na baadaye ASP Hafidhi na kuwaweka chini ya ulinzi, wakawahoji na kulifungua begi ambapo walikuta vitu hivyo.

Mpelelezi kutoka ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Sajenti Abogasti (46) alidai kuwa washtakiwa Bihagaze, Mzava na Milulu walipeleka silaha saa nane usiku katika Hospitali ya TMJ alipokuwa amelazwa Askofu Gwajima baada ya kubaini kwamba walikuwa nayo kinyume cha sheria.

FAMILIA YAGOMBEA MAITI KWA SIKU 12, SOMA HAPA

Mazishi ya Ernest Materego, yamekwama kwa siku 12 baada ya wanafamilia kufungua kesi mahakamani wakizozana sehemu ya kumzika.

Mvutano huo unawahusisha watoto wawili wa marehemu dhidi ya baba yao mdogo. Watoto wanataka baba yao azikwe Dar es Salaam huku baba yao mdogo akitaka azikwe Bunda mkoani Mara.

Watoto hao, Joyce na Edwin Materego wanaowakilishwa na Wakili Raymond Wawa, wamefungua shauri hilo wakati tayari mwili wa baba yao aliyefariki dunia jijini Dar es Salaam Novemba 19 ukiwa umesafirishwa Bunda tayari kwa mazishi.

Kesi hiyo iko mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya usuluhishi ulioendeshwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa kushindikana.

Watoto hao wanamlalamikia baba yao mdogo, Gonche Materego anayewakilishwa na Wakili Makaki Masatu kwamba amelazimisha baba yao akazikwe Bunda badala ya Dar es Salaam.

Joyce (45) aliiambia Mahakama kuwa yeye kwa sasa anaishi London, Uingereza na amefungua kesi hiyo na kaka yake wakiomba mahakama itoe amri ya kumzika baba yao Dar es Salaam.

Mtoto huyo alidai alifika nchini Novemba 23, 2016 kwa ajili ya kumzika baba yake aliyekuwa akiishi maeneo ya Ukonga, ambako aliwalea kama rafiki na kuzungumza naye mambo mengi.

Joyce alidai waliishi na baba yao katika mazingira ya dini ya Kikristo na kwamba aliwaambia endapo atakufa yeye au mama yao, wazikwe Dar es Salaam.

Akiongozwa na wakili Wawa, Joyce alidai kuwa baada ya baba yake kufariki dunia, kamati ya mazishi iliyoketi chini ya baba yao mdogo ilipanga mwili upelekwe kuzikwa Bunda, lakini wao hawakuridhika badala yake walitaka azikwe jijini Dar es Salaam walikoishi naye tangu mwaka 1974.

Pia, wanaomba wakabidhiwe kibali cha mazishi alichopewa baba yao mdogo kwa ajili ya kuendelea na shughuli za mazishi. Akijibu madai hayo, Gonche alidai marehemu kaka yake pia alikuwa akiishi Bunda wakati wa uhai wake, hivyo anatakiwa kuzikwa huko na si Dar es Salaam.

Wakili Masatu aliweka pingamizi akidai mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo kwa sababu inahusu masuala ya kimila, hivyo ifutwe lakini Wakili Wawa, alidai kuwa hoja iliyopo mahakamani si suala la kimila, bali wapi mwili wa marehemu ukazikwe. Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa leo.

MAGAZETI YA TANZANIA LEO JUMAMOSI, YASOME HAPA

Magazeti ya Leo Jumamosi ya Disemba 3

TAARIFA MPYA KUTOKA MAHAKAMANI ARUSHA KUHUSU MBUNGE GODBLESS LEMA, SOMA HAPA

Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imemnyima dhamana Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA) Godbless Lema. Mahakama hiyo imeeleza kuwa mawakili wamtuhumiwa huyo walipaswa kuonesha kusudio la kukata rufaa ndani ya siku10 kabla ya kukata rufaa.

Hii ni mara ya tano mbunge huyo anakosa dhamana mahakamani tangu alipokamatwa Novemba 3 mwaka huu akiwa mjini Dodoma na kusafirishwa hadi Arusha katika kesi ya uchochezi inayomkabili.

Katika kesi ya msingi lema anatuhumiwa kutoa maneno ya kichochezi dhidi ya Rais Magufuli kwa madai kuwa Mungu ndiye aliyemwambia maneno hayo wakati akiwa anaomba.

VIDEO.. MWANAMKE AUAWA NA JOKA LA AJABU, TAZAMA HAPA

MWILI WA MZEE PINDA WAANGWA DODOMA, SOMA HAPA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa jana aliongoza mamia ya waombolezaji kuaga mwili wa marehemu Mzee Xavery Pinda ambaye ni baba mzazi wa Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Mizengo Pinda.

VIOJA: WAKULIMA LINDI WAMNUNULIA 'MBUZI' JUICE NA SODA BAADA YA KUUZA KOROSHO, SOMA HAPA

 
KOROSHO

SHULE NYINGI BINAFSI KUFUNGWA, SOMA HAPA

RAI

SAKATA LA DANGOTE KAA LA MOTO, SOMA HAPA

DANGOTE

© Copyright Mwanahabari Huru | Designed By Peruzibongo.com
Back To Top